Sunday, January 29, 2017

YAJUE MAMBO YANAYOSABABISHA UMASIKINI.
1 uvivu , ikiwa wewe ni mtu wa kuona kila unachofanya ni kigumu na hutaweza basi jua unakaribisha umasikini katika maisha yako.
2 kukata tamaa, ukiwa mwenye kukata tamaa kwenye mambo yako jua kabisa jahazi la umasikini linakuandama hivyo chukua hatua haraka iwezekanavyo.
3 huna ndoto za kuwa tajiri, ndugu yangu matajiri wote dunia waliishi kwa ndoto za kuwa mabilionea na walitamani mambo mazuri hivyo ndoto hukufanya ufikie malengo yako hili ni jambo muhimu sana kwenye maisha yao.
4 matumizi mabaya ya fedha, ikiwa wewe hujui namna ya kutumia pesa yako na huku kipato chako kikiwa kidogo tu basi upo kwenye hatari kubwa ya kuwa masikini.
5 kutopenda kujifunza, Hakika kama kuna jambo watu wanakosea na kuwapelekea kuwa masikini ni wao kutopendelea kujifunza vitu vipya.
 Imeandaliwa na msami

No comments:

Post a Comment