Tuesday, January 31, 2017


💥 *HAMASA YA SIKU, FEB 1*

✨Uzoefu katika kile unachokifanya hauji kwa bahati mbaya, bali unakuja kwa kuweka nguvu nyingi za uzingativu (Focus) kwa jambo hilo unalolifanya kwa muda mrefu. Ukitaka kuwa mtaalamu uliyebobea katika jambo lolote, weka nguvu za uzingativu katika jambo hilo bila kuacha kila siku na utalifanikisha.  
   
✨Unaposikia _‘aisee fulani ni mzoefu wa kazi yake na inampa mafanikio,’_ tambua sio uzoefu wa miaka ila ni uzoefu wa kitaalamu. Unaweza ukawa katika kazi yako kwa muda mrefu ila kama hujifunzi, utakuwa sawa na mtu aliyeanza hiyo kazi leo.      

✨Jenga uzoefu kwenye kazi yako kwa kuamua kuweka nguvu za uzingativu hapo na kujifunza kwa uhakika. Hakuna ambacho utakikosa sana ikiwa utaamua kuweka nguvu zako nyingi kwa kile unachokifanya na kuacha kuruka ruka.

Kila la kheri.

No comments:

Post a Comment