💥 *HAMASA YA SIKU,DEC,26*
✨ Watu wote wenye mafanikio makubwa, wana mambo makubwa mawili yaliyo ndani mwao. *Kwanza, ni malengo waliyojiwekea.* *Pili, Shauku kubwa(burning desire) ya kufikia ndoto zao.*
Mambo hayo mawili ndiyo yanawapa chachu na nguvu kubwa ya kufikia mafanikio yao.
✨ Ni hali ya kawaida kabisa hata wewe, ukitaka kufanikiwa, ni lazima sana kuwa na malengo sahihi unayoyafatilia kila siku na shauku kubwa ya kufanikiwa. Ikiwa utakosa kitu kimoja kati ya hivyo, utakuwa upo kwenye wakati mgumu sana wa kufanikiwa au naweza kusema hutaweza kufanikiwa kabisa.
Kila la kheri,
- ,
No comments:
Post a Comment