Saturday, January 21, 2017
HAMASA YA SIKU.
✨ Kuna watu wanatabia ya kuamini kwamba kwa sababu jana hawakuweza kufanikiwa, basi hata leo au kesho hawawezi kufanikiwa. Hiyo ni imani mbovu na potofu ambayo unatakiwa kuwa nayo makini sana, vinginevyo itakukwamisha sana kufikia mafanikio yako.
✨ Kama una imani hii unatakiwa kutambua ya kwamba jana sio sawa na leo, leo ni siku nyingine mpya, hivyo huna ulazima sana wa kuendelea kuamini hicho unachotaka kukiamini. Maisha yanabadilika na fikra zinabadilika pia. Usiendelee kuamini kwamba utakufa maskini, anza kuamini wewe utakuwa ni mtu wa mafanikio makubwa.
Kila la kheri,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Msami
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment